Adam Mchomvu’s Ruge Lyrics

Sijawai muona na upara, punk, dredi kama Chege Hajawai vaa skin tight, Jeans shusha mlege Sijui fegi, bangi, shisha, henny, mbege Busara kila neno alikuwa habongi kibwege

Alikuwa mbongo clever, Kwaya, mixer reggea Mzalendo kweli kweli ngangaro si legelege Mamalkia wa nguvu, vipepeo kedekede Kapromote michezo labda kama hukua ready

R.U.G.E jina lake Ruge Alama alizoacha ni sifa tusizuge Kama taifa lazima nyufa tuzibe Usije dondoka ukuta uwazi vyetu waibe

Aliamini sanaa, wasanii na bidhaa Kwanza pata nafasi, jenga jina kuwa star Ongeza dhamani na nidhamu kwa mitaa Maintain status ndio business na chapaa

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze

Maneno yenye nidhamu kwa saiti ya upole Bila kulipa ada wengi tulipata shule Kwa makelele ya shangwe kama fiesta Aliona upande wa pili vipi wakitambua na fursa

Mdogo mdogo vijana wakapigwa msasa Bila kubagua dini, jinsia au siasa Ogopa Mungu na technologia Hicho ndicho ambacho alicho tuhusia

Najua wengi tu wameshakuimbia Wengine wana mengi wanataka kukuambia Ila ndo umeshatangulia Nenda, jasiri muongoza njia

Scofield, Big Joe anagugumia CMG kila siku twakuombea Yeah, najua tunafatia salam Kwa uncle KIBS zizi na kuendelea

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu Ili taifa liendelee ni lazima tuendeleze

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu

See Also  Jessica Van Vonderen Married, Wiki, Age, Height, Instagram, Bio - 10 Facts

Alikuwa ni baba Alikuwa mwalimu kwetu Alisimama kama nguzo yetu

Alikuwa ni baba Alisimama kama nguzo yetu

Lets take over the game

We will be happy to hear your thoughts

Leave a reply

Wasit
Logo